Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amtaka CAG kuchunguza ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Chato
Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amesema kuwa fedha ambazo zimelipwa kwa mkandarasi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato na ununuzi wa ndege za Bombardier na Boeing hazikuidhinisha na CAG.
Zitto Kabwe amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kuelezea Maazimio ya Kamati kuu ya ACT Wazalendo kuhusiana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini kwa sasa.
Ametoa
ufafanuzi kuwa Utaratibu unataka fedha kuingia kwenye
Mfuko Mkuu (Consolidated Fund) na kisha kuidhinishwa na CAG, na ndipo Serikali
kuanza kutumia.
Sanjari na
hayo amefafanua kuwa Shilingi bilioni 300 kutumika na
Serikali bila kushirikisha Bunge na kufuata sheria za nchi ni kusigina Katiba
na kudharau Taasisi za Uwajibikaji za nchi.
Aidha Kamati Kuu ya ACT Wazalendo imemtaka CAG afanye ukaguzi maalum wa fedha hizo na kutoa taarifa kwa Bunge ili sasa Bunge liweze kuiwajibisha na kuisimamia Serikali vizuri.
Source Eatv
Editor Alinanuswe Edward
Comments
Post a Comment