Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila ameidhinisha muswada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi, baada ya bunge na baraza la Seneti kutofautiana kuhusu yaliomo katika sheria hiyo.
Hatimae Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila ameidhinisha muswada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi, baada ya bunge na baraza la Seneti kutofautiana kuhusu yaliomo katika sheria hiyo.
Serikali inasemasheria hiyo mpya imekuja kutatua matatizo yaliojitokeza katika chaguzi zilizopita hususan kumaliza hali ya wabunge kuchaguliwa kwa kura chache.
Mbunge wa bunge la kitaifa sasa itabidi awe na asilimia moja ya wawakilishi ya kura zote alizopata.
Upinzani nchini humo unasema hatua hiyo itawanyima haki wagombea binafasi na kuwaondoa kabisa katika mchakato wa uchaguzi , kwa mujibu wa Christophe Lutundula mwenyekiti wa chama cha muungano kwa ajili ya maendeleo ambae pia ni naibu mwenyekiti wa muungano wa upinzani G7.
Msemaji wa muungano wa vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila (Majorite Presidentielle) André-Alain Atundi amepongeza hatua hiyo.
Mbali na sheria hiyo ya uchaguzi, rais Joseph Kabila ameidhinisha pia sheria ya bajeti ya mwaka 2018, ambayo ilikuwa ni kikwazo kikubwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) ili kuheshimu utekelezwaji wa kalenda ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka 2018.
Comments
Post a Comment