Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kufuta mifuko ya hifadhi ya jamii na kubakiza miwili.

DODOMA

Rais wa Tanzania Dk John  Pombe Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kufuta mifuko ya hifadhi ya jamii na kubakiza miwili.

Amesema mifuko itakayobaki ni kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi wa sekta binafsi na ya umma.

Rais Magufuli amesema Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) litabaki kwa ajili ya kuhudumia wafanyakazi wa sekta binafsi wakati mifuko mingine yote itaunganishwa na kuwa mmoja.

Amesema hayo alipofungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mjini Dodoma ambapo ameeleza kuwa mifuko hiyo imegeuka dili kwa vigogo ambao huamua kujenga majumba makubwa ili wapate asilimia 10.


Mifuko mingine inayotoa huduma ya hifadhi ya jamii ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.

Comments

Popular posts from this blog

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanao jiuza, na wanao vaa nusu utupu waanza kunywea maji kwenye karai Dar