MASHEHE WAJIUDHURU KATAVI

KATAVI

MASHEHE watano akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Katavi, Shehe Shaaban Bakari wamejiuzulu uongozi wakidai kuwepo kwa migogoro ya uongozi na ukiukwaji wa Katiba ya Bakwata.

Halmashauri ya baraza hilo inaundwa na viongozi sita ambao ni mashehe, watano kati yao ndio waliotangaza kujiuzulu ambao ni Mwenyekiti wao Shehe Bakari, Shehe Mashaka Kakulukulu, Shehe Hassan Mbaruku, Shehe Said Haruna Omary na Shehe Mohamed Sigulu.

Wakitangaza uamuzi huo  mbele ya waandishi wa habari, Shehe Kakulukulu amesema haoni sababu ya kuendelea kuwa kiongozi wa halmashauri ya baraza hilo akidai kumekuwepo na baadhi ya mambo ya kimaendeleo ambayo hayaendi sawa.

Kauli hiyo imeungwa mkono na mashehe wengine, huku Shehe Sigulu akidai kuwa msuguano uliopo wa kiuongozi ndani ya Bakwata umesababishwa na mwalimu wa madrasa katika Msikiti Mkuu mjini Mpanda kuamua kuacha kazi ya kufundisha hivi karibuni.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI