Kheri James atangazwa kuwa Mwenyekiti mpya UVCCM


Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa (UVCCM), leo umemtangaza Kheri James kuwa Mwenyekiti mpya atakayeongoza kwa miaka mitano.

Kheri ametangazwa mshindi baada ya kupata Kura 319 kati ya kura 583 zilizopigwa akiwashinda wenzake 6 aliokuwa akichuana nao kuwania nafasi hiyo. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imechukuliwa na Tabia Mwita.

Mkutano wa Uchaguzi wa UVCCM umefanyika mjini Dodoma kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ndiye aliye simamia uchaguzi huo na kumtangaza mshindi.


Mkutano huo wa uchaguzi wa UVCCM ulifunguliwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli na unafungwa leo na Rais wa Zanziobar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.