Zaidi ya wanafunzi 9000 mkoani Katavi kukosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya madalasa



KATAVI

Zaidi ya wanafunzi 9000 waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mkoani Katavi wamekosa nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa. 

Akitangaza matokeo ya mtihani huo katika kikao maalumu cha uchaguzi wa wanafunzi Afisa Elimu mkoa wa Katavi Ernest Hinju amesema jumla watahiniwa 7,190 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kutwa.

Aidha watahiniwa 162 hawakuweza kufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali hali iliyopelekea wadau wa elimu kujadili changamoto za kushuka kwa elimu, kwani kulinganisha na mwaka uliopita mkoa wa Katavi umeshika nafasi ya 9 kitaifa kutoka nafasi ya 2 mwaka uliopita 

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Katavi Bwana Gideon Marandu amezitaka halmashauri zote kuhakikisha wanafunzi waliokosa nafasi wanapata nafasi ifikapo Februari mwaka 2018


Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI