Mkoa wa Katavi umetengewa kiasi cha billion 14.392 kwaajili ya ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 68.60.

KATAVI

Na Alinanuswe Edward.



Mkoa wa Katavi umetengewa kiasi cha billion 14.392  kwaajili ya ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 68.60.

Kauli hiyo imetolewa leo Kaimu Meneja wa TANROAD Martin Mwakabende kwenye Uzinduzi wa utekelezaji wa kazi za matengenezo ya barabara ya mwakaa 2016/17 na mwaka 2017/18   katika kikao cha 10 cha Bodi ya Barabara ya mkoa wa Katavi(RRB).

Aidha ameongeza kusema kuwa Wameanza kuthibiti Magari mazito barabarani kutokana na  kuwa na mizani ya kuhamishika kwa lengo la kudhibiti uharibifu wa barabara..

Mgeni rasmi katika kikao hicho ambaye ni mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Mhuga amesisitiza uwajibikaji kwa vitendo ili kufikia malengo.


Katika utekelezaji wa Mradi huo wa matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2016/17 zilitengwa  sh.billioni  15.431 Na mwaka 2017/18  sh.billion 14.392 kwaajili ya ukarabati wa Barabara.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI