TUNDULISU ASIMAMA KWA MARA YA KWANZA TANGU KUPIGWA RISASI NA WATU WASIO JULIKANA
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Nairobi Kenya baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana, ameanza kusimama kwa mara ya kwanza kwa msaada wa madaktari.
Taarifa kutoka Hospitali ya Nairobi imeeleza kuwa Lissu kwa mara ya kwanza ameweza kusimama kwa msaada wa Physiotherapist tangu Septemba 7, mwaka huu alipopigwa risasi mjini Dodoma, hatua chache kabla ya kufika nyumbani kwake.
Akizungumza kutoka Hospitalini hapo, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanansheria Tanganyika (TLS), amesema "Wapendwa wote wiki iliyopita niliwataarifu kwamba madaktari wangu wamesema nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania"
"Leo Boxing Day nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa mababa cheza kama inavyoonekana, hatua inayofuata nitawajulisheni," Lissu
Comments
Post a Comment