TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru) inamshikilia aliyekuwa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba
DAR – ES
SALAAM.
TAASISI ya Kupambana na Kuzuia
Rushwa Tanzania (Takukuru) inamshikilia aliyekuwa Rais wa Chama cha Walimu
Tanzania (CWT), Gratian Mukoba kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa katika
uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.
Msemaji wa Takukuru, Mussa
Misalaba amesema, kwamba Mukoba amekamatwa
na maofisa wa uchunguzi wa taasisi hiyo kwenye viwanja
vya Chimwaga ambako uchaguzi huo ulikuwa unaendelea.
Misalaba alidai kwamba Rais
huyo wa zamani CWT alikuwa anajaribu kuwahonga wapiga kura.
Mukoba alichaguliwa kuwa
Makamu wa Rais wa CWT mwaka 2002 na mwaka 2007 alichaguliwa kuwa Rais wa chama
hicho, kabla ya mwaka 2014, kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Tanzania (Tucta). Na
kustaafu ualimu hivi karibuni.
Source EATV
Editor Alinanuswe Edward.
Comments
Post a Comment