Wakulima wa zao tumbaku mkoani Katavi wailaumu serikali kushindwa kutekeleza ahadi yake.

Katavi

Na Alinanuswe Edward.


Wakulima wa zao la tumbaku wa chama cha msingi cha ushirika Mpanda Kati Mkoani Katavi wameilaumu serikali kushindwa kutekeleza agizo lake la kuhakikisha tumbaku iliyo kosa soko inanunuliwa.

Wakulima hao  kwa nyakati tofauti wamesema mpaka sasa hawajui hatima ya ununuzi wa tumbaku yao huku wengine wakisema wameathirika kiuchumi na maisha kwa ujumla.

Hivi karibuni,mwenyekiti chama cha msingi cha Ushirika Mpanda Kati Bw.Sosipeter Salvatory ,alisema kuna kiasi cha tani elfu ishirini na mbili ambazo hazijanunuliwa kati ya kiasi chote cha tumbaku iliyozalishwa katika msimu wa mwaka  mwaka 2016/2017.


Mnamo Novemba 17 mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiahirisha vikao vya Bunge mjini Dodoma alieleza kuwepo kwa kampuni itakayo nunua Tumbaku iliyosalia pamoja na Mbaazi.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI