Vijana mkoa wa katavi wametakiwa kuungana katika uwajibikaji ili kujiletea maendeleo



Vijana mkoa wa katavi wametakiwa kuungana katika uwajibikaji ili kujiletea maendele na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa  umoja wa Vijana CCM (UVCCM) mapema leo alipokuwa akizungumza na Mpanda radio fm kwa njia ya simu akiwa mjini Dodoma kuhudhuria mkutano mkuu wa chama hicho.

Ameitaja shabaha kubwa kuwa ni kuwaunganisha vijana kupitia maendeleo na kwamba hii ndio itakuwa suruhu ya kuondoa migawanyiko miongoni mwao ambayo hushudiwa kwa kiwango cha juu katika vipindi vya uchaguzi.

 Aidha ameongeza kusema kuwa ilikufikia Tanzania ya viwanda  ni lazima vijana wote waelekeze nguvu zaidi katika Kilimo.


Wakati haya yakijiri Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Dk John Pombe Magufuli ameutaka umoja wa vijana UVCCM nchini kuwa na mawazo mapya yenye tija kwa jamii na taifa.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI