Posts

Showing posts from September, 2017

JESHI LA POLISI LIMEMUACHIA MSIGWA

Image
Peter Msigwa Mbunge wa Iringa mjini. Polisi mjini Iringa imemuachia mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa kwa sharti la kumtaka arudi polisi Jumatatu. Taarifa zinasema mbunge huyo ambae pia ni mchungaji wa kanisa alikamatwa pindi alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Mlandege huko Mkoani Iringa. Kwa mujibu wa msemaji wa Chadema Tumaini Makene, polisi inadai kumkatama Msigwa kwa tuhuma za uchochezi. Msingwa anatoka chama cha Chadema ambacho ndio chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania. Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na kamata kamata ya wabunge nchini Tanzania kutoka upinzani hasa Chadema. Miongoni mwa waliokumbwa na kamata hiyo hivi karibuni ni mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambae hivi sasa yuko nchini Kenya kwa ajili ya matibabu baada ya kupigwa risasi na watu ambao mpaka sasa hawajafahamika huko Dodoma, bungeni.

ABILIA WA TREN MPANDA WAKWAMA SIKU NZIMA

Image
Na, Issack Gerald Zaidi ya abiria 200 walikwama kusafiri siku ya jana kwa treni kutoka Mkoani Katavi kwenda mikoa mingine  wanatalajia kuondoka mapema leo. Inadaiwa kuwa kushindikana kwa safari siku ya jana kulitokana na uwepo wa hitilafu katika njia ya treeni maeneo ya mkoa wa Tabora. Baadhi ya abiria ambao walikuwa wakitegemea usafiri huo wamelalamika ubovu wa kichwa cha treni pamojana na kutopewa taarifa rasmi mara treni inapoharibika huku wakiathirika na njaa.   Tumekaa hapa tangu jana asubuhi na tulitalaji tuondoke jana hiyo hiyo alasili, hakuna taarifa yoyote tuliyopewa na uongozi badala yake tunaambiwa usiku kuwa kunatatizo, tunateseka na watoto.Amesikika mmoja wa abilia wa Treni hiyo akisema. Hata hivyo msemaji wa  kituo cha Treni Mpanda amekataa kutoa ushirikiano ili kueleza chanzo usumbufu huo unao jitokeza mara kwa mara.

DUNIA IPO KATIKA KITISHO KIKUBWA.

Image
Msitu wa Ikolongo ulio zunguka vyanzo va maji katika Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi NA Alinanuswe Edward. Hali ya uharibifu wa mazingira ni kitisho kikubwa kwa sasa katika dunia inayo pambana kujinasua na  majanga mbali mbali  yanayo sababishwa na shughuri  za kibinadamu. Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa inayotajwa kuwa kinara wa uharibifu huo hasa ukiwa ni ukataji wa misitu hovyo pamoja na uchomaji wa mkaa. Maeneo mengi  ya misitu yaliyo hifadhiwa  katika vyanzo  vya maji yameteketezwa kwa kuchomwa moto. Mto Ikolongo ambao ndio chanzo muhimu kinacho tumiwa na mamlaka ya Maji mkoa wa Katavi Muwasa. Mapema 2017 Mkuu wa wilya ya Tanganyika Salehe Muhando alianzisha mkakati kabambe wa kupambana na uharibifu wa mazingira unao fanywa na wakulima wa zao la mpunga ambao hufunga mto huo na kuchimba mifereji ya kutiririsha maji katika mashamba. Katika mahojiano alieleza shabaha yake kuwa ni kulinda mto huo usikauke ...

MBOWE; TUNDULISU HAPELEKWI POPOTE!

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe, amesema Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu hatosafirishwa kwenda popote mpaka pale madaktari watakaporuhusu. Mhe. Mbowe ameeleza hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari ikiwa imepita siku moja tokea serikali ya Tanzania itoe kauli yake kuwa ipo tayari kumtibia Lissu popote pale duniani kupitia Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu. "Tundu Lissu bado ni mgonjwa sana, hawezi kusafirishwa nje ama kutikiswa kwa njia yeyote katika kipindi hiki kwa hiyo mpango wowote wa kumuondoa hospitalini Nairobi kumpeleka nchi yeyote hautokuwepo kwa sasa mpaka hapo madaktari watakaporuhusu kulingana na hali yake",  amesema Mbowe. Pamoja na hayo, Mbowe ameendelea kwa kusema   "Madaktari wametuhakikishia wana vifaa, dawa,...

KAULI ZA MAREKANI ZINANISHAUWISHI KUTENGENEZA SIRAHA ZAIDI....

Image
Kim Jong-un amesema kauli za "wazimu'' rais wa Marekani Donald Trump zimemshawishi kuwa alikuwa sahihi kutengeneza silaha kwa ajili ya Korea kaskazini. Katika kauli yake binafsi ambayo haikutarajiwa, kupitia vyombo vya habari vya taifa, Bwana Kim alisema kuwa Bwana Trump ''atalipia" hotuba yake ya hivi karibuni katika Umoja wa Mataifa. Jumanne wiki hii rais wa Marekani alisema kwamba kama Marekani ikilazimishwa kujilinda ''itaiangamiza kabisa'' Korea Kaskazini. Bwana Trump pia alimkejeli Bwana Kim akimuita "rocket man" anae andaa mpango wa ''kujiangamiza ". Korea Kaskazini imekuwa ikifanya majaribio ya makombora, na ilifanya jaribio la sita la nuklia licha ya majaribio hayo kulaaniwa kimataifa.

SASA NIMETIMIZA WAJIBU WANGU...ZITTO

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kusema kwa sasa ametimiza wajibu wake kukutana na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na kuweza kutoa sababu zake kwanini anaamini Bunge linatumiwa na serikali na kuwa ni bunge lisilo na meno. Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe . Zitto Kabwe ambaye jana aliweza kukutana na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na kufanya mahojiano nao amesema kuwa kwa upande wake yeye ametimiza wajibu wake hivyo sasa kazi imebaki kwenye Kamati husika kupima maelezo yake na kile anachotuhumiwa na kufanya maamuzi, lakini pia amesema anaamini Kamati hiyo itafanya maamuzi kwa haki na bila ya kuwa na woga wala hofu.  "Nipo huru baada ya masaa 24 tangu nikamatwe na polisi Uwanja wa Ndege Dar es Salaam na kuletwa Dodoma kwa gari. Nimekutana na Kamati ya Bunge ya Kinga na Haki na kuhojiwa. Nimetoa maelezo yangu yenye lengo la kulinda Uhuru wa maoni na kulinda hadhi...

MITANDAO YA MAWASILIANO YA ONLINE YATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Image
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Kilimbe amesema lengo la serikali kuboresha sera na kanuni za mitandao ya kijamii ni kutaka kuweka usalama katika nchi pamoja na kutumiwa vyema ili iweze kuleta maendeleo. Dkt. Kilimbe amebainisha hayo wakati alipofungua warsha na vyombo vya habari vya mtandaoni 'online media' na kusisitizia kuwa kutokana na ukuaji wa mitandao ya kijamii ni vyema ikatumika vizuri na kuzingatia utu pamoja na staha. "Mawasialiano ya mtandao (online) yameendelea kukua mpaka sasa kuna 'online TV'  zaidi ya 50 na 'blogs' zaidi ya 150 huku TV zikiwa 32 tu hivyo ni vyema zikatumika vyema bila kufanya uchochezi wa aina yeyote",  amesema Dkt. Kilimbe. Aidha, Dkt. Kilimbe amesema kutokana na ukuaji wa mitandao ya kijamii umeweza kuonesha jinsi teknolojia ilivyopokelewa vizuri kwani taarifa zimeweza kupatikana kwa haraka endapo ukiwa na simu ya mkononi. "Kutoka...

KIWANDA CHA UPASUAJI MAGOGO KATIKA KATA YA MISUNKUMILO MKOA WA KATAVI CHENYE ZAIDI YA WAFANYAKA 20 HAKINA CHOO

Image
Kiwanda cha kupasulia magogo kilichopo kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda  mkoani Katavi  chenye zaidi ya wafanyakazi   20 hakina huduma ya choo. Wakizi wa eneo hilo ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema wanakabiliwa na harufu mbaya kwa muda mrefu kutokana watu kujisaidia hovyo katika maeneo hayo hasa shughuri zinapoendelea kufanyika katika kiwanda hicho. Mmiliki wa kiwanda hicho ambaye amejitambulisha kwa jina moja la Bilali amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuahidi kulipatia ufumbuzi ndani ya muda mfupi Aidha ameongeza kusema kuwa  kiwanda hicho kilisimama uzalishaji kutokana na serikali  kusitisha uvunaji wa bidhaa za misitu hivyo kuathiri shughuli za uendelezaji wa kiwanda hicho Serikali kupitia mmalaka zake imekuwa ikisisitiza ujenzi wa vyoo bora kati maeneo ya makazi na taasisi mbalimbali ili kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu.

WAKATI FUKUTO LA KISIASA LA KUTAKA KUONGEZWA MUDA WA UHAI WA BUNGE NA URAISI LIKIINYEMELEA TANZANIA UGANDA PIA HALI NI ILE ILE

Image
Rais wa Uganda Yoweri Museveni Meya wa mji mkuu wa Uganda Kampala amekamatwa leo asubuhi kwa madai ya kuandaa maandamano ya kupinga muswada mpya wa umri wa rais kugombea. Polisi inasema kuwa ilikuwa na taarifa kwamba Erias Lukwago angeongoza maandamano ya kupinga kikomo cha umri wa rais  kugombea . Kukamatwa kwa Meya Lukwago kunakuja wakati Mbunge Raphael Magyezi kutoka chama tawala cha NRM akitarajiwa kuwasilisha hoja yake bungeni akitaka apewe kipindi cha mapumziko kwa ajili ya kuandaa muswada wa kuondoa kikomo cha umri wa rais. Rais Yoweri Museveni anasema kuwa ana umri wa miaka 73. Hii ina maana kuwa, kwa sheria ilivyopo sasa ,hataweza kugombea katika uchaguzi ujao.

WATU 226 WAMEPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA TETEMEKO LA ARDHI

Watu 226 miongoni mwao watoto 25 wamepoteza maisha hadi sasa kufuatia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.1 katika kipimo cha Ritcher lililotokea nchini Mexico.  Zaidi ya nusu ya waliopoteza maisha kufuatia tetemeko hilo ni kutoka katika mji mkuu wa nchi hiyo Mexico City.  Vikosi vya uokozi viliendelea kuwatafuta manusura wa tukio hilo. Tetemeko hilo limetokea ikiwa ni karibu wiki mbili baada ya tetemeko lingine la ardhi kutokea kusini magharibi mwa nchi hiyo ambalo liliwaua takribani watu 90.

NI ZAIDI YA MWEZI MMOJA WALIO KUWA WAKAZI WA KITONGOJI CHA MGOLOKANI MKOA WA KATAVI WANAISHI CHINI YA MITI

Image
Hapa ni moja wapo ya makazi ya wahanga wa matukio ya kuchomwa kwa makazi yao kwa madai ya kuwa katika hifadhi za misitu. Na Alinanuswe Edward. Wakati wa uchaguzi wanasiasa walikuja kufanya kampeni huku huku wanakosema ni hifadhi tukaletewa masanduku ya kupigia kura, nashangaa leo hii tunateseka ndani ya nchi yetu wenyewe,, Amesikika  Maria Bernad mama wa mtoto mwenye umri wa miaka 2 akisema kwa uchungu. Zaidi ya mwezi mmoja sasa walio kuwa wakazi wa kitongoji cha Mgolokani kata ya Starike halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi  wanaishi chini ya miti tangu kufanyika kwa operesheni ya kuwaondoa wananchi katika maeneo yanayo daiwa kuwa hifadhi za misitu mkoani Katavi. Aliyekuwa Mwenyekiti wa kitongoji cha mgolokani Bw.Divason Kisulo  amesema tangu operesheni ifanyike ya kuondoa wananchi katika maeneo hayo hakuna sehemu mbadala iliyotengwa kwaajili ya makazi mapya. Awali Mkuu wa wilaya ya Mpanda B Lilian Matinga alikili kufanyika kwa operesheni hiyo kwa madai kuwa in...

BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LAIWEKEA VIKWAZO KOREA KASKAZINI

Image
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepiga kura kwa kauli moja kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini kama adhabu ya kufanyia majaribio zana zake za nuklia. Vikwazo hivyo vinalenga kuhujumu uwezo wa Pyongyang kufadhili na kutoa kawi kwa mpango wake wa nuklya. Vikwazo hivyo vilevile vinatoa masharti kwa biashara ya kununua mafuta ya Korea Kaskazini mbali na kupiga marufuku uuzaji wa nguo katika mataifa ya kigeni. Maamuzi hayo ya baraza la usalama la umoja wa mataifa yaliungwa mkono kwa wingi wa kura baada ya Marekani kuondoa mpango wake wa kutaka uungwaji mkono kutoka Urusi na China Korea Kusini inasema kuwa kwa kuhujumu amani Korea Ksakzini itaewekewa vikwazo zaidi vya kimataifa. Balozo wa China katika Umoja wa kimataifa Liu Jieyi ameitaka Korea kaskazini kuchukua kwa muhimu mkubwa matarajio ya ya jamii ya kimataifa na kuharibu mpango wa

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

Image
Zaidi ya wakazi 1000 wa kijiji cha Kabuga katika kata ya Kanoge mkoani Katavi wanakabiliwa na adha ya maji safi na salama. Baadhi ya Wanawake katika eneo hilo wamewalaumu viongozi wa kijiji hicho kutokana na kushindwa kutatua tatizo hilo, na wengine wamesikika wakisema walipewa ahadi hewa kipindi cha uchaguzi wa 2015. Miongoni mwao wameeleza kuwa utawala wa serikali ya kijiji hicho, umeingiza udanganyifu hata katika mambo ya msingi kama vile huduma za kijamii. j Mwandishi wa habari Alinanuswe Edward akimhoji mkazi wa kijiji cha Kabuga katika kisima cha maji kinachotumika na wakazi wa eneo hilo "Tulifanya makosa kipindi cha uchaguzi kwa kuchagua viongozi wasio weza kututekelezea mahitaji yetu Nathaniel hili ni funzo zote kwetu"Amesema Mama Rozi katika mahojiano. Mwenyekiti wa kijiji hicho Benjamini Ezekiel amekili kuwepo kwa tatizo hilo na kueleza jitihada za serikali kuwa ni kuongeza idadi ya vizima ili viweze kukidhi mahitaji ya wakazi. Lakini visa ...

Waziri aunga mkono ndoa ya jinsia moja

Image
Viongozi wa siasa nchini Australia akiwemo waziri mkuu Malcolm Turnbull, wameunga mkono kampeni inayopigia debe ndoa ya jinsia moja. Zaidi ya watu 20,000 walikusanyika mjini Sydney kwenye kampeni kabla ya kura ya maoni isiyo rasmi ya kubadilishwa sheria za ndoa nchini Australia. Bwana Turnbull alijitokeza kwa ghafla na kutoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo huko New South Wales. Kiongozi wa upinzani Bill Shorten kisha akahutubia umati kwenye mkutano mkuu. Kura hiyo ya kubadilisha sheria ya ndoa inapigwa kwa njia ya posta kuanzia Septemba 12 na matokeo yakitarajiwa mwezi Novemba. Kura hiyo haitakuwa na uwezo wa kuhalalisha ndoa ya jinsia moja, lakini itachangia kura kupigwa bungeni ikiwa asilimia kubwa na watu nchini Australia wataunga mkono mabadiliko hayo. Awali waziri mkuu alisema kuwa yeye binafs...

Wazari aunga mkono ndoa za jinsia moja

Image
Viongozi wa siasa nchini Australia akiwemo waziri mkuu Malcolm Turnbull, wameunga mkono kampeni inayopigia debe ndoa ya jinsia moja. Zaidi ya watu 20,000 walikusanyika mjini Sydney kwenye kampeni kabla ya kura ya maoni isiyo rasmi ya kubadilishwa sheria za ndoa nchini Australia. Bwana Turnbull alijitokeza kwa ghafla na kutoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo huko New South Wales. Kiongozi wa upinzani Bill Shorten kisha akahutubia umati kwenye mkutano mkuu. Kura hiyo ya kubadilisha sheria ya ndoa inapigwa kwa njia ya posta kuanzia Septemba 12 na matokeo yakitarajiwa mwezi Novemba. Kura hiyo haitakuwa na uwezo wa kuhalalisha ndoa ya jinsia moja, lakini itachangia kura kupigwa bungeni ikiwa asilimia kubwa na watu nchini Australia wataunga mkono mabadiliko hayo. Awali waziri mkuu alisema kuwa yeye binafsi ...

LISU APIGWA RISASI

Image
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma. Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea. Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.

PANGA LA JPM SASA LAANZA KAZI YAKE BAADA YA KIMYA CHA MUDA MREFU

Image
Muda Mfupi baada ya Raisi Magufuli kusema wateule wake waliotajwa katika  taarifa ya uchunguzi wa madini ya Tanzanaiti na Almasi  wakae pembeni  ili kupisha uchunguzi wa kina  baadhi ya viongozi hao wameanza kuandika barua za kuachia nyadhifa zao.  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa huo baada ya kutajwa katika ripoti hizo zilizoonyesha namna serikali lilivyopoteza matrilioni ya fedha kutokana na sababu mbalimbali. Mbali na Simbachawene pia Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani ameandika  barua ya kujiuzulu wadhifa wake.

Walio husika na skendo ya Almasi na Tanzanite sasa wapigwa kadi nyekundu.

Image
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DK John Pombe Magufuli ameaviagiza vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuwachukulia hatua vigogo wote walio tajwa katika ripoti ya madini ya Almasi na Tanzanite. Raisi Magufuli ametoa agizo hilo  leo Ikulu jijini Dar-es salaam wakati akipokea taarifa ya uchunguzi wa madini ya Tanzanaiti na Almasi  kutoka kwa waziri Mkuu uliofanywa na kamati mbili za bunge zilizoundwa na Spika wa bunge Job Ndungai. Katika kuanza kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na kamati hizo mbili kuwawajibisha watendaji wa serikali waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za madini Raisi magufulu amesema wateule wake waliotajwa wakae pembeni  ili kupisha uchunguzi wa kina  ufanyike na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa dhidi yao. Aidha Raisi Magufuli amesistiza suala la uzalendo kwa watanzania wote hasa wale viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi.   

Wananchi walalamikia mapato na matumizi Uyui mkoani Tabora

Image
picha na grobalpublishers Na Mussa Mbeho ,Tabora. Serikali ya kijiji cha Itobela kata ya Ibelamilundi  wilayani Uyui Mkoani Tabora imelalamikiwa kwa kutokutoa taarifa ya mchanganuo wa pesa ambazo ni zaidi ya shilingi milioni Moja na Lakini Saba zinazotolewa na chama cha msingi kila mwaka kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya kijiji hicho. Wakizungumza na mpanda  fm leo   baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamesema kuwa  ni miaka miwili sasa wamekuwa wakiomba mchanganuo wa fedha hizo lakini viongozi wa serikali ya kijiji wamekuwa wakigoma kutoa taarifa juu ya fedha hizo. Kutokana na malalamiko hayo ya wananchi mpanda fm imemtafuta Diwani wa kata ya Ibelamilundi Bwana Maiko Jemsi ili kujua ufatiliaji wa suala hilo. Akijibu malalamiko hayo  mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Itobela bwana Juma Magembe amesema kuwa fedha hizo zipo kwenye akaunti ya serikali ya kijiji nakuahidi kuwa ndani ya mwezi huu ataitisha mkutan...

Kimbunga kikali kwa Jina Irma kimesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Caribbean ambapo takriban watu saba wameuawa.

Image
Kisiwa kidogo cha Barbuda kilisemekana kukumbwa na uharibifu mkubwa hadi kutajwa kuwa kisichoweza kukalika huku maafisa wakionya kuwa himaya ya Uingereza ya St Martin imeharibiwa kabisa. Kimbunga Irma chasababisha uharibifu mkubwa Jitihada za uokoaji zinatatizwa kutokana na kuwepo ugumu wa kuyafikia maene mengine. Haki miliki ya picha AFP Image caption Kimbunga Irma kimesababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean Wakati huo huo upepo umetajwa kupata nguvu na kuwa vimbunga viwili. Kimbunga Irma cha kiwango cha tano, ambacho ni kiwango cha juu zaidi kwa sasa kinapita kaskazini mwa Puerto Rico. Watu wafanya maandalizi ya mwisho kabla kuwasili kimbunga Irma Zaidi ya nusu ya wakaazi wote milioni tatu wa Puerto Rico hawana umeme baaada ya kimbunga Irma kusababisha mvua kubwa na upepo mkali. Maafiasa wanasema huenda umeme ukakosa kwa siku kadhaa. Haki miliki ya picha AFP Image caption Kimbunga Irma kimesababisha uharibifu mkubwa huko Caribbean Kimbunga hicho chenye nguvu nying...

Ekari 100 za tengwa Rukwa kwaajili ya ujenzi wa Hosipital

Image
Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 100 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya. Kwa sasa taratibu za ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi huo zinakamilika na serikali itawalipa fidia stahiki wahusika. Akijibu swali bungeni leo , Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo  amesema kwa sasa wagonjwa wanapata huduma katika hospitali teule iliyopo pamoja na vituo vya Afya na zahanati. Katika swali la msingi, mbunge wa viti maalumu Bupe Mwakang'ata  (Chadema), ametaka kujua  ni lini serikali itajenga hospitali ya wilaya katika wilaya za Nkasi na Sumbawanga ambako wanawake wanapata shida. "Serikali itajitahidi kutafuta fedha na kushirikiana na wananchi wa Nkasi ili kufanikisha ujenzi wa hospitali ya wilaya," amesema Jafo. Kuhusu hospitali ya rufaa alisema Mkoa wa Rukwa umeanza taratibu za ujenzi wa hospitali katika eneo la Milanzi ambapo hospitali inayotumika kwa sasa itabaki kuwa hospitali ya...

Raila Odinga apinga tarehe mpya ya uchaguzi Kenya

Image
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kuwa hayuko tayari kushiriki marudio ya uchaguzi mkuu wa urais nchini humo. Bwana Odinga amesema kuwa anataka kuwepo mikakati ya kisheria na kikatiba inayohitajika, kabla ya yeye kukubali kushiriki uchaguzi huo. Bwana Odinga pia anataka mabadiliko kufanyiwa Tume ya uchaguzi nchini humo, ambayo imelaumiwa na mahakama ya juu kwa wa kuendesha uchaguzi kwa njia ambayo haiukuwa nzuri ambayo ilisababisha kufutiliwa mbali matokeo. Jana Jumatatu Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya ilitangaza kwamba uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba. Source BBC Swahili.