Walio husika na skendo ya Almasi na Tanzanite sasa wapigwa kadi nyekundu.
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DK John Pombe Magufuli ameaviagiza vyombo
vya ulinzi na usalama nchini kuwachukulia hatua vigogo wote walio tajwa katika
ripoti ya madini ya Almasi na Tanzanite.
Raisi Magufuli ametoa agizo
hilo leo Ikulu jijini Dar-es salaam
wakati akipokea taarifa ya uchunguzi wa madini ya Tanzanaiti na Almasi kutoka kwa waziri Mkuu uliofanywa na kamati
mbili za bunge zilizoundwa na Spika wa bunge Job Ndungai.
Katika kuanza kutekeleza
mapendekezo yaliyotolewa na kamati hizo mbili kuwawajibisha watendaji wa
serikali waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za madini Raisi magufulu
amesema wateule wake waliotajwa wakae pembeni
ili kupisha uchunguzi wa kina
ufanyike na kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa dhidi yao.
Aidha Raisi Magufuli amesistiza
suala la uzalendo kwa watanzania wote hasa wale viongozi waliopewa dhamana ya
kusimamia rasilimali za nchi.
Comments
Post a Comment