PANGA LA JPM SASA LAANZA KAZI YAKE BAADA YA KIMYA CHA MUDA MREFU






Muda Mfupi baada ya Raisi Magufuli kusema wateule wake waliotajwa katika  taarifa ya uchunguzi wa madini ya Tanzanaiti na Almasi  wakae pembeni  ili kupisha uchunguzi wa kina  baadhi ya viongozi hao wameanza kuandika barua za kuachia nyadhifa zao. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa huo baada ya kutajwa katika ripoti hizo zilizoonyesha namna serikali lilivyopoteza matrilioni ya fedha kutokana na sababu mbalimbali.

Mbali na Simbachawene pia Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani ameandika  barua ya kujiuzulu wadhifa wake.



Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI