KIWANDA CHA UPASUAJI MAGOGO KATIKA KATA YA MISUNKUMILO MKOA WA KATAVI CHENYE ZAIDI YA WAFANYAKA 20 HAKINA CHOO
Kiwanda
cha kupasulia magogo kilichopo kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi
chenye zaidi ya wafanyakazi 20
hakina huduma ya choo.
Wakizi
wa eneo hilo ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema wanakabiliwa na harufu
mbaya kwa muda mrefu kutokana watu kujisaidia hovyo katika maeneo hayo hasa
shughuri zinapoendelea kufanyika katika kiwanda hicho.
Mmiliki
wa kiwanda hicho ambaye amejitambulisha kwa jina moja la Bilali amekiri kuwepo
kwa tatizo hilo na kuahidi kulipatia ufumbuzi ndani ya muda mfupi
Aidha
ameongeza kusema kuwa kiwanda hicho
kilisimama uzalishaji kutokana na serikali
kusitisha uvunaji wa bidhaa za misitu hivyo kuathiri shughuli za
uendelezaji wa kiwanda hicho
Serikali
kupitia mmalaka zake imekuwa ikisisitiza ujenzi wa vyoo bora kati maeneo ya
makazi na taasisi mbalimbali ili kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko kama
kipindu pindu.
Comments
Post a Comment