WAKATI FUKUTO LA KISIASA LA KUTAKA KUONGEZWA MUDA WA UHAI WA BUNGE NA URAISI LIKIINYEMELEA TANZANIA UGANDA PIA HALI NI ILE ILE



Rais wa Uganda Yoweri Museveni


Meya wa mji mkuu wa Uganda Kampala amekamatwa leo asubuhi kwa madai ya kuandaa maandamano ya kupinga muswada mpya wa umri wa rais kugombea.

Polisi inasema kuwa ilikuwa na taarifa kwamba Erias Lukwago angeongoza maandamano ya kupinga kikomo cha umri wa rais  kugombea .

Kukamatwa kwa Meya Lukwago kunakuja wakati Mbunge Raphael Magyezi kutoka chama tawala cha NRM akitarajiwa kuwasilisha hoja yake bungeni akitaka apewe kipindi cha mapumziko kwa ajili ya kuandaa muswada wa kuondoa kikomo cha umri wa rais.


Rais Yoweri Museveni anasema kuwa ana umri wa miaka 73. Hii ina maana kuwa, kwa sheria ilivyopo sasa ,hataweza kugombea katika uchaguzi ujao.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.