NI ZAIDI YA MWEZI MMOJA WALIO KUWA WAKAZI WA KITONGOJI CHA MGOLOKANI MKOA WA KATAVI WANAISHI CHINI YA MITI
Hapa ni moja wapo ya makazi ya wahanga wa matukio ya kuchomwa kwa makazi yao kwa madai ya kuwa katika hifadhi za misitu. |
Wakati wa uchaguzi wanasiasa walikuja kufanya kampeni huku huku wanakosema ni hifadhi tukaletewa masanduku ya kupigia kura, nashangaa leo hii tunateseka ndani ya nchi yetu wenyewe,,Amesikika Maria Bernad mama wa mtoto mwenye umri wa miaka 2 akisema kwa uchungu.
Zaidi ya mwezi mmoja sasa walio kuwa wakazi wa kitongoji cha Mgolokani kata ya Starike halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wanaishi chini ya miti tangu kufanyika kwa operesheni ya kuwaondoa wananchi katika maeneo yanayo daiwa kuwa hifadhi za misitu mkoani Katavi.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa kitongoji cha mgolokani Bw.Divason Kisulo amesema tangu operesheni ifanyike ya kuondoa wananchi katika maeneo hayo hakuna sehemu mbadala iliyotengwa kwaajili ya makazi mapya.
Awali Mkuu wa wilaya ya Mpanda B Lilian Matinga alikili kufanyika kwa operesheni hiyo kwa madai kuwa inafanywa katika maeneo ambayo wananchi wamevamia misitu.
Zoezi hilo linalofanywa katika Wilaya ya Mpanda na Mlele mkoani Katavi limewaacha mamia ya wakazi bila mahala pa kuishi.
Comments
Post a Comment