Ekari 100 za tengwa Rukwa kwaajili ya ujenzi wa Hosipital



Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 100 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Kwa sasa taratibu za ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi huo zinakamilika na serikali itawalipa fidia stahiki wahusika.
Akijibu swali bungeni leo , Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo  amesema kwa sasa wagonjwa wanapata huduma katika hospitali teule iliyopo pamoja na vituo vya Afya na zahanati.
Katika swali la msingi, mbunge wa viti maalumu Bupe Mwakang'ata  (Chadema), ametaka kujua  ni lini serikali itajenga hospitali ya wilaya katika wilaya za Nkasi na Sumbawanga ambako wanawake wanapata shida.
"Serikali itajitahidi kutafuta fedha na kushirikiana na wananchi wa Nkasi ili kufanikisha ujenzi wa hospitali ya wilaya," amesema Jafo.
Kuhusu hospitali ya rufaa alisema Mkoa wa Rukwa umeanza taratibu za ujenzi wa hospitali katika eneo la Milanzi ambapo hospitali inayotumika kwa sasa itabaki kuwa hospitali ya wilaya ya Sumbawanga.



Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI