DUNIA IPO KATIKA KITISHO KIKUBWA.
Msitu wa Ikolongo ulio zunguka vyanzo va maji katika Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi |
NA Alinanuswe Edward.
Hali ya uharibifu wa mazingira ni kitisho kikubwa kwa sasa
katika dunia inayo pambana kujinasua na
majanga mbali mbali yanayo
sababishwa na shughuri za kibinadamu.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa inayotajwa kuwa kinara
wa uharibifu huo hasa ukiwa ni ukataji wa misitu hovyo pamoja na uchomaji wa
mkaa.
Maeneo mengi ya misitu
yaliyo hifadhiwa katika vyanzo vya maji yameteketezwa kwa kuchomwa moto.
Mto Ikolongo ambao ndio chanzo muhimu kinacho tumiwa na mamlaka ya Maji mkoa wa Katavi Muwasa. |
Mapema 2017 Mkuu wa wilya ya Tanganyika Salehe Muhando
alianzisha mkakati kabambe wa kupambana na uharibifu wa mazingira unao fanywa
na wakulima wa zao la mpunga ambao hufunga mto huo na kuchimba mifereji ya
kutiririsha maji katika mashamba.
Katika mahojiano alieleza shabaha yake kuwa ni kulinda mto
huo usikauke na kupotea hasa kutokana na ukweli kwamba bila uwepo wa mto huo
huenda kikawa ndio kiama cha hifadhi ya taifa ya Katavi ambayo hupitiwa na mto
huo.
Katika kipindi chote hicho idara ya misitu na mali asili
zimeshutumiwa vikali na wadau wa mazingira wakiwemo wananchi kutokana na
kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Hili ni eneo lililo karibu kabisa na Barabara ya Mpanda mjini kuelekea Tanganyika licha ya kuwepo kwa onyo bado limechomwa moto. |
Utafiti uliofanywa ulibainisha kuwa baadhi ya wanasiasa wametumika pakubwa
katika kuhatarisha mazingira kwa kuwalaghai wananchi kuyatumia maeneo hayo,
wakati mwingine kuwalinda wakulima wakubwa kwa hongo.
Comments
Post a Comment