WATU 226 WAMEPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA TETEMEKO LA ARDHI
Watu 226 miongoni mwao watoto 25 wamepoteza maisha hadi sasa kufuatia tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.1 katika kipimo cha Ritcher lililotokea nchini Mexico.
Zaidi ya nusu ya waliopoteza maisha kufuatia tetemeko hilo ni kutoka katika mji mkuu wa nchi hiyo Mexico City.
Vikosi vya uokozi viliendelea kuwatafuta manusura wa tukio hilo. Tetemeko hilo limetokea ikiwa ni karibu wiki mbili baada ya tetemeko lingine la ardhi kutokea kusini magharibi mwa nchi hiyo ambalo liliwaua takribani watu 90.

Comments
Post a Comment