Wananchi walalamikia mapato na matumizi Uyui mkoani Tabora

picha na grobalpublishers





Na Mussa Mbeho ,Tabora.

Serikali ya kijiji cha Itobela kata ya Ibelamilundi  wilayani Uyui Mkoani Tabora imelalamikiwa kwa kutokutoa taarifa ya mchanganuo wa pesa ambazo ni zaidi ya shilingi milioni Moja na Lakini Saba zinazotolewa na chama cha msingi kila mwaka kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya kijiji hicho.

Wakizungumza na mpanda  fm leo   baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamesema kuwa  ni miaka miwili sasa wamekuwa wakiomba mchanganuo wa fedha hizo lakini viongozi wa serikali ya kijiji wamekuwa wakigoma kutoa taarifa juu ya fedha hizo.

Kutokana na malalamiko hayo ya wananchi mpanda fm imemtafuta Diwani wa kata ya Ibelamilundi Bwana Maiko Jemsi ili kujua ufatiliaji wa suala hilo.

Akijibu malalamiko hayo  mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Itobela bwana Juma Magembe amesema kuwa fedha hizo zipo kwenye akaunti ya serikali ya kijiji nakuahidi kuwa ndani ya mwezi huu ataitisha mkutano wa hadhara ili kuwapa Taarifa wananchi juu ya fedha hizo.

Hata Hivyo wakazi wa kijiji hicho wamewaomba viongozi wa serikali ya kijiji kubadilika na kusikiliza maoni yao ili kuweza kuleta maendeleo  katika  kijiji hicho.


Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI