ABILIA WA TREN MPANDA WAKWAMA SIKU NZIMA

Na, Issack Gerald

Zaidi ya abiria 200 walikwama kusafiri siku ya jana kwa treni kutoka Mkoani Katavi kwenda mikoa mingine  wanatalajia kuondoka mapema leo.

Inadaiwa kuwa kushindikana kwa safari siku ya jana kulitokana na uwepo wa hitilafu katika njia ya treeni maeneo ya mkoa wa Tabora.

Baadhi ya abiria ambao walikuwa wakitegemea usafiri huo wamelalamika ubovu wa kichwa cha treni pamojana na kutopewa taarifa rasmi mara treni inapoharibika huku wakiathirika na njaa.

 Tumekaa hapa tangu jana asubuhi na tulitalaji tuondoke jana hiyo hiyo alasili, hakuna taarifa yoyote tuliyopewa na uongozi badala yake tunaambiwa usiku kuwa kunatatizo, tunateseka na watoto.Amesikika mmoja wa abilia wa Treni hiyo akisema.


Hata hivyo msemaji wa  kituo cha Treni Mpanda amekataa kutoa ushirikiano ili kueleza chanzo usumbufu huo unao jitokeza mara kwa mara.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI