MAHAKAMA HAINA RAFIKI
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amewataka viongozi wa vyama siasa kuacha tabia ya kufikilia vibaya Mahakama kuwa haiwatendei haki pindi wanapokuwa na kesi zao Mahakamani. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole. Polepole ameeleza hayo baada ya kushinda kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu ya mwaka 2015 kwa upande wa Ubunge katika jimbo la Longido Mkoani Arusha ambalo lilikuwa likigombewa baina ya Dkt. Steven Kiruswa kutoka CCM na Onesmo Nangole kutoka CHADEMA. "Sisi kama chama cha Mapinduzi tumepokea uamuzi huo kwa faraja kubwa kwa sababu hivi karibuni kulikuwa na maneno kutoka kwa waakilishi wa vyama vya siasa vingine siyo vyote. Ambavyo vyenyewe huwa vinaamini kuwa Mahakama ikitoa haki kwao inakuwa imewatendea haki ila Mahakama ikitoa haki kwa wengine inakuwa haitendi haki. Sisi kama Chama cha Mapinduzi tunaamini Mahakama ipo pale ilipo kwa ajil...