WANDISHI WA HABARI WAPATA MSASA WA TEHAMA
Wandishi wa habari katika redio jamii nchini wametakiwa kuanza kuwekeza katika matumizi ya mitandao ya kijamii katika kutoa taarifa .
Baadhi ya washiriki wakifuatlia kwa umakini matumizi ya vifaa mbali mbali vya kimtandao. |
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kituo cha Kahama Fm radio James Lembel wakati akifungua mafunzo ya siku tisa kwa waandishi wa habari vituo vya redio za kijamii yaliyofanyika katika ukumbi wa Kartasi ya kanisa la Katholic uliopo mjini Kahama mkoani Shinyanga.
"Ninaimani kuwa endapo mtajitoa na kutumia fursa za mafunzo haya vizuri mtaifikia jamii iliyo kusudiwa na kuisaidia katika nyanja mbali mbali kama vile uwajibikaji"Amesema Lembeli.
Aliye simama Kati kati ni aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini James Lembeli, kulia ni Mkufunzi mwandamizi wa UNESCO Rozi Mwalimu na aliye kushoto mwishoni ni Sebastian Okiki. |
Kwa upande wa muwezeshaji
mkuu wa mafunzo hayo kutoka UNESCO Rozi Mwalimu ametoa rai kwa washiriki kuanza
mkakati wa kuuhabarisha umma kidijitali kwa kutumia mitandao ya kijamii
kutokana na ukuaji wa mifumo ya mawasiliano.
Comments
Post a Comment