BAADHI YA MAWAKILI WAMGOMEA LISU

Baadhi ya mawakili katika Mahakama ya Mkazi Kisutu wakiwa Kazini.
Baadhi ya Mawakili wameendelea na shunghuli zao za uwakili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam mapema leo.
Licha ya kuwepo kwa wito wa Rais wa chama cha Mawakili Tanzania (TLS) Tundu Lisu kuwataka mawakili wote nchini kususia shughuli za Mahakama kwa muda wa siku Mbili (Jumanne na Jumatano) kufuatia Ofisi za Mawakili IMMMA ADVOCATES kupigwa Mabomu na watu wasiojulikana mapema mwishoni mwa wiki iliopita jijini Dar es salaam.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limesemakwamba linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini watu hao waliofanya tukio hilo pamoja na kujua dhamira yao ili wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.
Mapema baada ya kutokea kwa mashambulizi hayo, Kaimui Jaji Mkuu pamoja na Jeshi la Polisi walionya Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS), kwa kuingilia uchunguzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi.By Habari Leo

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI