Chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Katavi kimelaani kitendo cha uchomaji wa makazi ya watu wanaodhaniwa kuwa wanaishi katika hifadhi ya misitu na kuitaka serikali kutafakari upya suala hilo.
Akizungumza na mpanda radio fm mapema leo Katibu wa chama hicho mkoa wa Katavi Bw Joseph Mona ameiambia mpanda radio kuwa visa vya uchomaji wa makazi ya wananchi katika vitongoji kadhaa na kuwaacha bila mahali pakuishi ni suala lisilo kubalika.
Sanjari na hayo ameeleza kuwa mkakati wa chama hicho wa kuishauri serikali ikiwemo kuikosoa umepelekea kuwasilisha ajenda kadhaa za wananchi katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jeneral mstaafu Raphael Muhuga kwa ufumbuzi wa tatizo hilo.
Mwanzoni mwa mwezi huu Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matinga ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mpanda amekili kufanyika kwa zoezi hilo kwa madai kuwa limefanywa katika maeneo ambayo wananchi wamevamia misitu.
Mwishoni mwamwezi jully 2017 Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DK John Pombe Magufuli akiwa katika ziara mkoani Tabora aliwa waagiza watendaji kutumia utu wanapo waondoa wananchi katika maeneo yasiyo kuwa makazi.
Watetezi wa haki za binadamu pamoja na wanaharakati wanasema kuwa huruma na utu dhidi ya ubinadamu vimetenganishwa na ukuta wa chuma kiasi cha kutoona madhara yanayoweza kujitokeza kwa familia hizo.
Vitongoji vilivyo kumbwa na kadhia ya kuchomewa makazi ni Kitongoji cha Nsanda kilichopo kata ya Kanoge, Makutanio na Mgolokani katika kata ya Stalike ambapo mamia ya wakazi wanaishi chini ya miti na familia zao.
Comments
Post a Comment