Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesimikwa rasmi kuwa chifu wa kabila la Wasafwa linalopatikana katika mkoa wa Mbeya . Dkt. Ndugulile amesimikwa uchifu huo wakati wa ziara yake mkoani Mbeya yenye lengo la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao. Dkt. Ndugulile amesema kuwa Wizara yake imeamua kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi za Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushiriki kwa vitendo kwa kufanya kazi na jamii kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, kilimo, barabara, viwanda na maji, nk. Ameongeza kuwa lengo la ziara hiyo ni kufuatilia namna ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii ambayo inasisitiza ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli au miradi ya maendeleo ikiwemo upanuzi na uendelezaji wa miundo mbinu mijini na vijijini kama Shule, Barabara, Zaha...
Comments
Post a Comment