Imebainika kuwa Wazazi na
Walezi mkoani Katavi ni chanzo cha uwepo wa ndoa nyingi katika umri mdogo.
Hayo yamebainishwa na
mwangalizi na mtetezi wa haki za binadamu kwa mikoa ya Katavi na Tabora
Kusundwa Wamarwa alipokuwa akizungumza na Mpanda radio fm amesema suala hilo
limeshamiri zaidi vijijini.
Aidha ameongeza kusema
kuwa upo mpango wa kuendelea kutoa elimu ya malezi katika ngazi ya familia kwa
kushirikiana na jeshi la Polisi kupitia
kitengo cha Dawati la jinsia na watoto pamoja na kamati za vijiji.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) imesema mkoa wa Katavi ndio unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya
wasichana wanaopata mimba wakiwa na umri mdogo kwa asilimia 36.8, mikoa mingine ni Tabora
36.5 na Simiyu 32.1 huku Dar es Salaam ukiwa mwishoni kwa asilimia 12.
.
Comments
Post a Comment