Zaidi watu 250 wameuawa kwenye maporomoko ya ardhi Sierra Leone .
Shirika la habari la AP linasema kuwa takriban watu 250 wameuawa.
Makamu wa rais nchini Sierra Leone Victor Bockarie Foh, alisema kuwa kuna uwezekano kuwa mamia ya watu wameuawa akiongeza kwa idadi ya watu waliouawa huenda ikaongezeka.
Mwandishi wa habari aliye eneo hilo anasema kuwa watu wemgi walipatwa wakiwa bado wamelala wakati maporomoko yalitokea
"Mke wangu amekufa, watoto wangu wote wamekufa, Leo asubuhi niliongea na watoto wangu kabla ya kuenda kazini. Mmoja wao hata alinipa soksi nilizovaa." alisema mwathiriwa mmoja.
"Tulikuwa ndani, tukaskjia udongo ukikaribia, tukajaribu kukimbia, nilijaribu kumchukua mtoto wangu, lakini udongo ulikuja kwa haraka sana . Alifukiwa akiwa hai. Sijamuona mume wangu. Mtot wangu alikuwa na umri wa wiki saba." alisema muathiriwa mwingine.
Maafisa wanasema kuwa ni mapema sana kutoa idadi kamili ya watu waliouawa
Comments
Post a Comment