MADARASA YA SHULE YA MSINGI NSANDA ILIYOPO HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI YABAKIA KUWA MAGOFU
Tumetumia nguvu kubwa kujenga shule hii kwa hisani ya Serikali ya watu wa Uingereza pamoja na shirika la Wakimbizi UNHCR, kwa usimamizi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania sasa majengo haya yaliyojengwa kisasa yanabakia kuwa magofu! tunaenda wapi jamani,,amesema Paulo Johnson katika mahojiano huku akibubujikwa na machozi.
Paulo Johnson akihojiwa na mwandishi wetu Alinanuswe Edward |
Safari yangu imeanzia katika shule ya Msingi Nsanda iliyopo Kasikazini mwa mkoa wa Katavi ulio kusini magharibi mwa Tanzania.
Hili ni bango nnje ya madarasa ya shule ya msingi Nsanda iliyopo kata ya Kanoge halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi. |
Eneo la shule hiyo yenye majengo ya kisasa limebakia tupu,
Kwambali ni vyoo vya shule ya msingi Nsanda. |
Makazi ya wananchi katika eneo hili yameharibiwa kabisa kwa kuchomwa moto na mamlaka ya misitu kwa kile kinachodaiwa kuwa ni sehemu ya hifadhi ya misitu.
kilomita tano kutoka katika eneo hilo nimeshuhudia mamia ya wakazi wakiwa wameweka kambi chini ya miti pamoja na familia zao.
Mama moja amesema hali ni mbaya anahofia kuwapoteza watoto wake kutokana na magonjwa.
Kwa upande wa mkuu wa wilaya ya Mpanda ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Bi Lilian Matinga mapema mwanzoni mwa mwezi agost alikili kuwaondoa wakazi katika maeneo hayo kwa kile alichokiita kuwa wamevamia maeneo hayo na kwamba ni hatari katika ustawi wa mazingira.
Comments
Post a Comment