Posts

Showing posts from November, 2017

Mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe ametoa wito akitaka makamu wa rais mwenye ushawishi kutimuliwa kutoka kwa chama cha Zanu-PF, kabla ya mkutano wake wa mwezi ujao, kwa mujibu wa gazeti la Herald.

Image
Mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe ametoa wito akitaka makamu wa rais mwenye ushawishi kutimuliwa kutoka kwa chama cha Zanu-PF, kabla ya mkutano wake wa mwezi ujao, kwa mujibu wa gazeti la Herald. Matamshi yake yanakuja siku moja baada ya Rais Robert Mugabe, 93, kutisha kumfuta Bw Mnangagwa, hatua ambayo imezua uvumi kuwa anataka mke wake amrithi. Akihutubia wanachama wa makanisa ya asili mji Harare siku ya Jumapili, Bi Mugabe alisema: "Nyoka ni lazima apiwe kwenye kichwa. Lazima tukabiliane na nyoka mwenyewe anayehusika na migawanyiko chamani.Tuneelekea kwenye mkutano tukiwa chama kimoja. Bi Mugabe ambaye ni mkuu wa Zanu-PF kitengo cha wanawake, na Bw. Mnangagwa wanaonekana kama wagombea wakuu katika jitihada za kumrithi Bw. Mugabe wakati atakufa au kuondoka madarakani. Haki miliki ya picha AFP Image caption Robert Mugabe Matamshi yake yalikuja baada ya wafuasi wa Bw. Mnangagwa kumkemea wakati wa mkutano uliofanyika mjini Bulawayo. Rais Mugabe alijibu kwa hasira...

Wanawake 26 wa Nigeria wafa maji katika bahari ya Mediterranean

Image
Miili ya wanawake 26, inayoaminika kuwa ya raia wa Nigeria, imepatikana katika ufukwe wa bahari nje kidogo ya pwani ya Italia. Wanawake hao, ambapo mdogo zaidi kwa umri anaaminika kuwa wa miaka 14, walikuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kutokea Libya ili kuingia Bara Ulaya. Haijabainika mara moja kiini kilichosababisha wanawake wengi kiasi hicho kufa kwa wakati mmoja, kwani kulikuwepo pia na wanaume kwenye meli iliyokuwa ikiwasafirisha. Kuna shaka kuwa, huenda walibakwa na kisha kuuwawa, walipokuwa wakivuka kupitia njia hiyo hatari ya bahari ya Mediterranean. Waendesha mashtaka nchini Italia, kwa sasa wanachunguza kubaini kiini hasa kilichosababisha maafa hayo, kwani wanawahoji wahamiaji watano katika mji wa bandarini wa Salerno ulioko Kusini mwa Italia.

MBINU YA KUIVAMIA KOREA KASKAZINI

Image
Maafisa kutoka makao makuu ya ulinzi nchini Marekani, wanaamini kuwa uvamizi wa kutumia vikosi vya Marekani vya nchi kavu, itakua njia pekee ya kupata na kudhibiti maeneo ya nyuklia ya Korea Kaskazini. Ripoti hiyo ilikuja kwenye barua iliyotolea na makao makuu ya ulinzi nchini Marekani, kujibu ombi la bunge la kutaka kufahamu kuhusu maafa yanayoweza kutokea ikiwa mzozo utalipuka na Korea Kaskazini Pia barua hiyo pia ilionya kuwa Korea Kaskazini anaweza kugeuka na kuwa eneo lenye silaha za kibaolojia na kemikali wakati wa vita.

Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imesitisha mishahara ya walimu 15 ambao waligoma kuripoti vituo vipya vya kazi

MOROGORO Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imesitisha mishahara ya walimu 15 ambao waligoma kuripoti vituo vipya vya kazi baada ya kupewa uhamisho bila kulipwa posho zao za uhamisho. Akizungumza katika Mkutano wa Chama Cha Walimu (CWT) leo Novemba 5 wilayani humo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Kilosa, Noel Abeid amekiri kuzuia mishahara hiyo ili kushinikiza walimu hao kuripoti vituo vipya walivyopangiwa kwani vina uhitaji mkubwa. Chama cha Walimu wilayani Kilosa kimelalamikia vitendo vya watumishi kuhamisha walimu bila ya kupewa stahiki zao na wanapodai wanazuiliwa mishahara yao.  Awali iliagiza hakuna mtumishi wa serikali kuhamishwa bila kulipwa stahiki zake za uhamisho lakini agizo hilo linakiukwa na uong hao 150.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameweka jiwe la msingi katika Uwanja wa Ndege wa Chato

GEITA Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameweka jiwe la msingi katika Uwanja wa Ndege wa Chato wenye kiwango cha daraja la 4C ambao ujenzi wake utagharimu Sh39.15 bilioni. Akizungumza katika haflahiyo, Profesa Mbarawa amesema kiwanja hicho kinajengwa na mkandarasi Mtanzania kwa kiwango cha kimataifa. Waziri Mbarawa alisema katika awamu hii ya tano, wizara imeboresha na kuimarisha ujenzi katika viwanja vya ndege vya Lindi, Iringa, Moshi na Simiyu na katika bajeti ya mwaka 2017/18 Serikali imepanga kufanya upembuzi katika viwanja vya Iringa, Musoma na Songea na sasa wanatafuta makandarasi. Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato Septemba 2016 na mpaka sasa umeshajengwa kwa asilimia 52 na unategemewa kuchochea shughuli za maendeleo wilayani Chato na Mkoa wa Geita kwa jumla.

WANANCHI WATOA PONGEZI KWA JESHI LA POLISI -KATAVI

Image
KAMANDA WA JESHI LA  POLISI MKOA WA KATAVI DAMAS NYANDA NA. Alinanuswe Edward. Baadhi ya wakazi wa Kata ya Inteka iliyopo wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wamelipongeza jeshi la Polisi kwa kuimarisha ulinzi katika eneo hilo. Wakizungumza na Mpanda radio fm kwa nyakati tofauti wamesema ujenzi wa kituo cha kidogo cha polisi katika eneo hilo umepelekea kupungua kwa matukio ya uharifu tofauti na hapo awali. Katika hatua nyingine wameliomba jeshi la polisi, kuongeza askari wengine kutokana na ongezeko la wakazi  katika kata hiyo. Kata ya Itenka ni miongoni mwa maeneo ambayo hapo awali yalikuwa yakikumbwa na vitendo vya mauaji ya mara kwa mara ikiwemo vitendo vingine vya kiuhalifu.  

MWANAUME MMOJA NCHINI PAKISTAN AFUNGWA MIEZI SITA JELA KWA KUOA ,MKE WA PILI BILA IDHINI YA MKE WAKE

Image
Mahakama nchini Pakistan imemfunga mwanamume mmoja miezi sita jela ya kuoa mke wa pili bila ya idhini kutoka kwa mke wake. Mahakama hiyo ya mjini Lahore pia ilimuamrisha Shahzad Saqib, kulipa faini ya dola 1,900, na kukataa maoni yake kuwa dini ya kiislamu inamruhusu kuoa hadi wake wanne. Mke wa kwanza wa Sadiq Ayesha Bibi, alikuwa amefanikiwa kujitetea kuwa kuoa bila idhini yake ulikuwa ni ukiukaji wa sheria za familia nchini Pakistan. Wanaharakati wa masuala ya wanawake wanasema kuwa kesi hiyo ni pigo kwa ndoa za wake wengi na pia inafungua fulsa kwa wanawake kuifanya mahakama kuwa kimbilio.

HALIMASHAURI YA NSIMBO YA NUSURIKA KUVUNJWA

Image
NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI JOSEPH KAKUNDA Na: Alinanuswe Edward. Uongozi wa Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi umetakiwa kujitathimini kutokana na kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya mapato ya ndani. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa TAMISEMI Joseph Kakunda mara baada ya kupokea ripoti ya mkoa wa Katavi kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga. Aidha amefafanua kuwa serikali haitashindwa kuchukua hatua kwa watendaji wakuu wa halmashauri hiyo endapo hakutakuwa na mabadiliko ya haraka. Kwa mujibu wa Ripoti hiyo halmashauri hiyo ilikusanya mapato yake kwa 63% kinyume na agizo la Serikali ambayo inaagiza kufutwa kwa  halmashauri yoyote itakayo shindwa kufikia kiwango cha 80% kwa makusanyo yake.

Mahakama imemfutia kesi ya shambulio iliyokuwa ikimkabili Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima

Image
Siku sita baada ya Adam Malima kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mahakama imemfutia kesi ya shambulio iliyokuwa ikimkabili. Rais John Magufuli, Alhamisi Oktoba 26,2017 alifanya uteuzi mbalimbali ukiwemo wa wakuu wa mikoa. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatano Novemba 1,2017 imeifuta kesi dhidi ya Malima na mwenzake. Malima ambaye amesharipoti mkoani Mara hakuwepo mahakamani wakati uamuzi huo ukitolewa. Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage ameifuta kesi hiyo na kuwaachia huru washtakiwa baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuomba ifutwe. Chini ya kifungu cha 91 (1) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Mutalemwa ameomba shauri lifutwe kwa sababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi ya washtakiwa. Baada ya ombi hilo kuwasilishwa, Hakimu Mwijage alimuhoji Mutalemwa iwapo kuna sababu ya kuifuta kesi hiyo na kama hana hataifuta. Wakili Mutalemwa alisoma kifungu hicho akisema kinampa mamlaka DPP kuiondoa kes...

Museveni atishia kuwakamata madaktari iwapo watagoma

Image
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amewaambia wanachama wa muungano wa madaktari nchini humo kwamba ataitisha hali ya dharura na kuwakamata madaktari wote iwapo wataendelea na mpango wao wa kufanya mgomo wa kitaifa wiki ijayo. Daktari Ekwaro Obuku, kiongozi wa muungano huo amesema kuwa rais Museveni alimuonya na wenzake kwamba ataitisha hali ya dharura na kuwakamata madaktari wote iwapo watafanya mgomo huo siku ya Jumatatu. Lakini katibu wa maswala ya habari katika afisi ya rais Museveni amekana kutolewa kwa vitisho hivyo na kusisitiza kuwa mkutano huo ulikuwa mzuri. Daktari Obuku anasema kuwa wasiwasi wa rais ulionyesha umuhimu wa madaktari hao. Kulingana na daktari huyo rais Museveni aliwaahidi kutathmini upya mishahara ya madaktari na kufanya mikutano zaidi kuhusu swala hilo. Muungano huo sasa utapiga kura nyengine siku ya Jumatatu kuona iwapo wataendelea na mgomo huo.

Imeelezwa kuwa ukosefu wa mabweni katika shule ya sekondari Ndevelwa iliyoko katika halmashuri ya manispaa ya Tabora ni chanzo cha utoro kwa wanafunzi wa shule hiyo

Imeelezwa kuwa ukosefu wa mabweni katika shule ya sekondari Ndevelwa iliyoko katika halmashuri ya manispaa ya Tabora ni chanzo cha utoro kwa wanafunzi wa shule hiyo Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Martini Masashua Wakati akizungumza na Storm fm ofisini kwake Amesema kuwa sababu kubwa inayopelekea  wanafunzi kuwa watoro katika shule  hiyo ni ukosefu wa mabweni kwani wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutoka majumbani mwao mpaka mahali ambapo shule ilipo. Mariamu juma ni mama wa watoto wawili yeye ni mwanafuzi aliekatishwa masomo katika shule ya sekondari Ndevelwa kutokana na kutembea umbali mrefu hapa aneleza namna ambavyo alishawishika na hatimae kupata ujauzito . Nae Diwani wa Kata ya Ndevelwa Bwana Selemani Maganga amesema kuwa suala la ukosefu wa mabweni katika shule hiyo tayari amekwisha liwasilisha kwa mkurugenzi wa manispaa kupitia vikao vya baraza la madiwani. Kwa upande wake afisa elimu sekondari manispaa ya Tabora Mwa...

WANANCHI WANAO VAMIA MISITU WAPEWA ONYO MKOANI KATAVI

Image
Wakazi wa mkoa wa katavi wametakiwa kuacha tabia ya kuvamia misitu na kufanya shughuli katika hifadhi ambazo zinaweza kuharibu uoto wa asili. Hayo yamesemwa na samwel matula meneja wa misitu (TFS) kanda maalum ya mkoa wa Katavi wakati akizungumza na mpanda redio na kusema hakuna ruhusa ya watu kufanya shughuli kama kilimo au kuweka makazi katika hifadhi zilizopo katika maeneo mbalimbali. Hata hivyo meneja misitu wilaya ya mpanda Mustafa Abedi amewataka wale wote walioondolewa katika maeneo ya misitu kufuatia operesheni iliyofanyika mwezi wa saba kutorudi katika maeneo hayo na sheria kali zitachukuliwa kwa atakayekiuka agizo hilo. Mwezi wa saba operesheni ya kuwaondoa watu katika maeneo ya misitu kama vile msitu wa msaginya ,na misitu north east mpanda ilifanyika kwa lengo la kulinda misitu iliyopo katavi kwa manufaa ya wananchi wote

Mshambuliaji awaua watu 8 kwa kuwagonga kwa gari New York

Image
Meya wa mji wa New York, Bill De Blasio, amearifu kwamba watu 8 wamefariki dunia na zaidi ya 12 wamejeruhiwa na gari iliyowagonga waendesha baiskeli mjini humo. Bill amelielezea tukio hilo kuwa la ugaidi lililosababisha hofu mjini humo. Kamishna wa polisi wa jiji wa New York, James O'Neill, amemuelezea mtu aliyewtekeleza tukio hilo kuwa ni kijana wa miaka 29 aliyekuwa anaendesha gari ndogo la kubebea mizigo alilokuwa amelikodi. Alisema gari hilo liliwagonga watembea kwa miguu na wapanda baiskeli kabla ya kugongana na basi la shule. Kwa upande wake bwana O'Neill, amesema kuwa dereva wa gari hilo alitoka ndani ya gari lake na kuanza kuandaa silaha mbili kwa ajili ya shambulizi na kabla ya hilo, polisi walimuwahi na kumpiga risasi zilizomjeruhii. Polisi mjini humo wametoa tamko kwamba wanalichukulia tukio hilo kama shambulizi la kigaidi , Mtuhumiwa wa tukio hilo alichukuliwa na polisi kwa mahojiano zaidi ambao walithibitisha taarifa hizo katika kituo cha Lower Manhat...