Mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe ametoa wito akitaka makamu wa rais mwenye ushawishi kutimuliwa kutoka kwa chama cha Zanu-PF, kabla ya mkutano wake wa mwezi ujao, kwa mujibu wa gazeti la Herald.
Mke wa rais wa Zimbabwe Grace Mugabe ametoa wito akitaka makamu wa rais mwenye ushawishi kutimuliwa kutoka kwa chama cha Zanu-PF, kabla ya mkutano wake wa mwezi ujao, kwa mujibu wa gazeti la Herald.
Matamshi yake yanakuja siku moja baada ya Rais Robert Mugabe, 93, kutisha kumfuta Bw Mnangagwa, hatua ambayo imezua uvumi kuwa anataka mke wake amrithi.
Akihutubia wanachama wa makanisa ya asili mji Harare siku ya Jumapili, Bi Mugabe alisema:
"Nyoka ni lazima apiwe kwenye kichwa. Lazima tukabiliane na nyoka mwenyewe anayehusika na migawanyiko chamani.Tuneelekea kwenye mkutano tukiwa chama kimoja.
Bi Mugabe ambaye ni mkuu wa Zanu-PF kitengo cha wanawake, na Bw. Mnangagwa wanaonekana kama wagombea wakuu katika jitihada za kumrithi Bw. Mugabe wakati atakufa au kuondoka madarakani.
Matamshi yake yalikuja baada ya wafuasi wa Bw. Mnangagwa kumkemea wakati wa mkutano uliofanyika mjini Bulawayo.
Rais Mugabe alijibu kwa hasira akisema kuwa hawezi kamwe kuvumilia matusi ya mara kwa mara kutoka kwa wafuasi wa makamu wa rais.
Alimtaka Bw. Mnangagwa na wafuasi wake kumuonyesha uzalendo au afutwe kazi.
Zanu-PF kinatarajiwa kuifanyia mabadiliko katiba yake wakati wa mkutano na kuweka nafasi mbili za makamu wa rais moja ikiwa ni ya mwanamke.
Nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa na Bi Mugabe na kuongeza uwezekano wa kumrithi mume wake.
Comments
Post a Comment