Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameweka jiwe la msingi katika Uwanja wa Ndege wa Chato

GEITA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameweka jiwe la msingi katika Uwanja wa Ndege wa Chato wenye kiwango cha daraja la 4C ambao ujenzi wake utagharimu Sh39.15 bilioni.

Akizungumza katika haflahiyo, Profesa Mbarawa amesema kiwanja hicho kinajengwa na mkandarasi Mtanzania kwa kiwango cha kimataifa.

Waziri Mbarawa alisema katika awamu hii ya tano, wizara imeboresha na kuimarisha ujenzi katika viwanja vya ndege vya Lindi, Iringa, Moshi na Simiyu na katika bajeti ya mwaka 2017/18 Serikali imepanga kufanya upembuzi katika viwanja vya Iringa, Musoma na Songea na sasa wanatafuta makandarasi.


Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato Septemba 2016 na mpaka sasa umeshajengwa kwa asilimia 52 na unategemewa kuchochea shughuli za maendeleo wilayani Chato na Mkoa wa Geita kwa jumla.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI