Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imesitisha mishahara ya walimu 15 ambao waligoma kuripoti vituo vipya vya kazi

MOROGORO

Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imesitisha mishahara ya walimu 15 ambao waligoma kuripoti vituo vipya vya kazi baada ya kupewa uhamisho bila kulipwa posho zao za uhamisho.

Akizungumza katika Mkutano wa Chama Cha Walimu (CWT) leo Novemba 5 wilayani humo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Kilosa, Noel Abeid amekiri kuzuia mishahara hiyo ili kushinikiza walimu hao kuripoti vituo vipya walivyopangiwa kwani vina uhitaji mkubwa.

Chama cha Walimu wilayani Kilosa kimelalamikia vitendo vya watumishi kuhamisha walimu bila ya kupewa stahiki zao na wanapodai wanazuiliwa mishahara yao.


 Awali iliagiza hakuna mtumishi wa serikali kuhamishwa bila kulipwa stahiki zake za uhamisho lakini agizo hilo linakiukwa na uong hao 150.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI