WANANCHI WANAO VAMIA MISITU WAPEWA ONYO MKOANI KATAVI
Wakazi wa mkoa wa
katavi wametakiwa kuacha tabia ya kuvamia misitu na kufanya shughuli katika
hifadhi ambazo zinaweza kuharibu uoto wa asili.
Hayo yamesemwa na
samwel matula meneja wa misitu (TFS) kanda maalum ya mkoa wa Katavi wakati
akizungumza na mpanda redio na kusema hakuna ruhusa ya watu kufanya shughuli
kama kilimo au kuweka makazi katika hifadhi zilizopo katika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo meneja
misitu wilaya ya mpanda Mustafa Abedi amewataka wale wote walioondolewa katika
maeneo ya misitu kufuatia operesheni iliyofanyika mwezi wa saba kutorudi katika
maeneo hayo na sheria kali zitachukuliwa kwa atakayekiuka agizo hilo.
Mwezi wa saba operesheni ya kuwaondoa watu katika
maeneo ya misitu kama vile msitu wa msaginya ,na misitu north east mpanda
ilifanyika kwa lengo la kulinda misitu iliyopo katavi kwa manufaa ya wananchi
wote
Comments
Post a Comment