Imeelezwa kuwa ukosefu wa mabweni katika shule ya sekondari Ndevelwa iliyoko katika halmashuri ya manispaa ya Tabora ni chanzo cha utoro kwa wanafunzi wa shule hiyo
Imeelezwa kuwa ukosefu wa mabweni katika shule ya sekondari Ndevelwa iliyoko katika halmashuri ya manispaa ya Tabora ni chanzo cha utoro kwa wanafunzi wa shule hiyo
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Martini Masashua Wakati akizungumza na Storm fm ofisini kwake
Amesema kuwa sababu kubwa inayopelekea wanafunzi kuwa watoro katika shule hiyo ni ukosefu wa mabweni kwani wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutoka majumbani mwao mpaka mahali ambapo shule ilipo.
Mariamu juma ni mama wa watoto wawili yeye ni mwanafuzi aliekatishwa masomo katika shule ya sekondari Ndevelwa kutokana na kutembea umbali mrefu hapa aneleza namna ambavyo alishawishika na hatimae kupata ujauzito .
Nae Diwani wa Kata ya Ndevelwa Bwana Selemani Maganga amesema kuwa suala la ukosefu wa mabweni katika shule hiyo tayari amekwisha liwasilisha kwa mkurugenzi wa manispaa kupitia vikao vya baraza la madiwani.
Kwa upande wake afisa elimu sekondari manispaa ya Tabora Mwalimu Chata Luleka amesema jumla ya wanafunzi 343 hawakumaliza kidato cha 4 mwaka jana kwa sababu mbalimbali.
Comments
Post a Comment