WANANCHI WATOA PONGEZI KWA JESHI LA POLISI -KATAVI

KAMANDA WA JESHI LA  POLISI MKOA WA KATAVI DAMAS NYANDA



NA. Alinanuswe Edward.

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Inteka iliyopo wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wamelipongeza jeshi la Polisi kwa kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.

Wakizungumza na Mpanda radio fm kwa nyakati tofauti wamesema ujenzi wa kituo cha kidogo cha polisi katika eneo hilo umepelekea kupungua kwa matukio ya uharifu tofauti na hapo awali.

Katika hatua nyingine wameliomba jeshi la polisi, kuongeza askari wengine kutokana na ongezeko la wakazi  katika kata hiyo.

Kata ya Itenka ni miongoni mwa maeneo ambayo hapo awali yalikuwa yakikumbwa na vitendo vya mauaji ya mara kwa mara ikiwemo vitendo vingine vya kiuhalifu.


 

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.