HALIMASHAURI YA NSIMBO YA NUSURIKA KUVUNJWA
NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI JOSEPH KAKUNDA |
Na: Alinanuswe Edward.
Uongozi wa Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi umetakiwa
kujitathimini kutokana na kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya mapato ya
ndani.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa TAMISEMI Joseph
Kakunda mara
baada ya kupokea ripoti ya mkoa wa Katavi kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa Meja
Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga.
Aidha amefafanua kuwa serikali haitashindwa kuchukua hatua
kwa watendaji wakuu wa halmashauri hiyo endapo hakutakuwa na mabadiliko ya
haraka.
Kwa mujibu wa Ripoti hiyo halmashauri hiyo ilikusanya mapato
yake kwa 63% kinyume na agizo la Serikali ambayo inaagiza kufutwa kwa halmashauri yoyote itakayo shindwa kufikia
kiwango cha 80% kwa makusanyo yake.
Comments
Post a Comment