TANZANIA YAENDELEA KUKAA KILELENI
Rais wa Tnzania Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na Romania
wamekubaliana kuongeza wigo wa ufadhili wa masomo hususani katika fani za
udaktari na ufamasia ambapo Romania imekubali kutoa nafasi kumi (10) za masomo
kwa wanafunziwa Tanzania.
Rais Samia, akizungumza na waandishi wa habari leo amesema
Serikali za mataifa hayo mawili zimezungumzia fursa zilizopo katika sekta
za afya na utengenezaji wa dawa,kubadilishana uzoefu katika sekta ya kilimo
ikiwemo usindikaji wa mazao na kukabiliana na majanga.
Wakati huo huo, Tanzania nayo imetoa nafasi tano za ufadhili kwa
vijana wa Romania kuja kusoma kwenye vyuo watakavyovichagua ikiwa ni fursa ya
kuchangia jitihada za Serikali za kujengea uwezo, rasilimali watu na kuimarisha
huduma katika sekta mbalimbali.
Akizungumzia mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi wa COP28, 2023
Rais Samia amesema Tanzania inatarajia kuweka nguvu suala la nishati na nishati
safi ya kupikia, hivyo amemuomba Rais Iohannis kuiunga mkono Tanzania.
Rais Iohannis yupo nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku nne yenye
lengo la kuimarisha uhusiano baina ya nchi yake na Tanzania uliodumu kwa miaka
62 na ikiwa ni ziara ya kwanza kwa Mkuu wa Nchi kutoka Jamhuri ya Romania
kutembelea nchini.
Comments
Post a Comment