MCHUNGAJI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA NSIMBO APEWA SAA 24 KUONDOKA



Mchungaji wa Kanisa la ufufuo na Uzima ambaye ni mwangalizi wa kanda ya Nsimbo Lameki Monde aliyedai kufufua marehemu katika Kata ya Stalike amepewa saa 24 za kuondoka katika eneo hilo.

Afisa mtendaji wa Kata ya Stalike akizungumza kwa njia ya simu bila kutaja jina lake amethibitisha suala na kusema kuwa limezua taharuki miongoni mwa wananchi.

Mchungaji Lameki Monde amesema amealikwa na familia ya Marehemu Raymond Mirambo aliyefariki miezi miwili iliyopita  kifo ambacho mchungaji huyo anasema ni chakutatanisha.


Ndugu wa marehemu wanasema waliamua kumuita mchungaji huyo ili afanye maombezi yatakayo saidia kuonekana kimuuujiza kwa mtu huyo.

Wakazi wa kata  hiyo wamekumbwa na taharuki hasa kutokana na kuenea kwa taarifa hizo.

Comments

Popular posts from this blog

DKT.NDUGULILE ATAWAZWA KUWA CHIFU MWANYINGA WA KABILA LA WASAFWA MKOANI MBEYA

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI