Wafanyabiashara wa Samaki katika Ziwa Tanganyika waitaka serikali kubadili mwelekeo



TANGANYIKA:
Wafanyabiashara wa samaki katika soko la Mwaloni kata ya Ikola wilaya ya Tanganyika  wamaeiomba serikali kuimarisha huduma ya usafiri ziwa Tanganyika ili kuchochea ukuaji wa biashara ya  samaki.

Wameeleza kuwa ili kuwe na tija zaidi nilazima  ukuaji wa teknolojia ya masuala ya uvuvi iende sambamba na usalama wa vyombo vya usafirishaji majini.

Uchakavu wa barabara ya Ikola  yenye urefu wa km 125 mpaka Mpanda mjini ambapo ni kitovu cha soko la biashara ya samaki kinatajwa kuwa kikwazo cha maendeleo ya wakazi wa kata hiyo ambao hutegemea uvuvi.

Haya yote yanajiri ikiwa nisiku chache tangu Mkuu wa mkoa wa Katavi meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga  kueleza nia ya serikali ya kuanzisha uwekezaji wa kisasa katika mwambao wa ziwa hilo ili kuongeza thamani ya Samaki kabla ya kuuzwa.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.