Wito umetolewa kwa wanaume kujenga utamaduni wa kuwasindikiza wake zao kwenda kiliniki ili kuendana na sera ya afya ya uzazi kitaifa inayomtaka baba kushiriki katika kiliniki ya mama na mtoto wakati wote wa ujauzito mapaka kujifungua.
ISAAC
ARON ISAAC
KIGOMA:
Wito umetolewa kwa
wanaume kujenga utamaduni wa kuwasindikiza wake zao kwenda kiliniki ili
kuendana na sera ya afya ya uzazi kitaifa inayomtaka baba kushiriki katika
kiliniki ya mama na mtoto wakati wote wa
ujauzito mapaka kujifungua.
miongoni mwa akina baba
ambao wameunga mkono sera ya afya ya kushiriki kliniki ni Fedrick Joseph mkazi
wa wilaya ya kasulu mkoa wa kigoma amesema kuwa swala la afya ni mhimu sana
huku wakiwataka akina baba kulinda afya ya wake zao hasa kushiriki katika
kiliniki ya mama, baba na mtoto.
Na kwaupande wake
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Nyanyunsi Wilayani kasulu DKT Tobiasi Sigwejo
amesema kuwa kila mwanaume anatakiwa kuambatana na mke wake ili kujua afya yake
ingwa bado Elimu ni kidogo sana miongoni mwa jamii jambo linalokwamisha mpango
wa kiliniki ya baba, mama na mtoto.

Comments
Post a Comment