Waziri wa mambo ya nje wa China aanza ziara yake barani Afrika
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri
wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China iko tayari kuimarisha
mawasiliano na Rwanda katika nyanja mbalimbali kutoka uongozi hadi utamaduni.
Bw. Wang sasa yuko ziarani barani Afrika, ambako Rwanda ni kituo
cha kwanza katika ziara hiyo. Jana alipokutana na rais Paul Kagame wa Rwanda,
mjini Kigali, Bw. Wang alipongeza uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili
unaotokana na maelewano, kuaminiana na kuungana mkono kwa muda mrefu.
Amesema Rwanda imejipatia njia ya maendeleo endelevu inayoungwa
mkono na wananchi wake, na kwamba China inapenda kuimarisha mawasiliano na
Rwanda katika uzoefu wa uongozi wa nchi na kuzidisha hali ya kuaminiana
kisiasa.
Kwa upande wake, rais Kagame alisema Afrika inaiamini China na
inapenda kuona China ikifanya kazi muhimu zaidi barani humo. Ameishukuru China
kutokana na uungaji mkono na mchango wake kwa maendeleo ya Rwanda.
Wakati huohuo, kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya
kukutana na rais Kagame, Bw. Wang amesema mawaziri wa mambo ya nje wa China
wanaichukulia Afrika kuwa ya kwanza katika ziara ya kila mwaka, hii inaonesha
kuwa Afrika siku zote ni kipaumbele cha diplomasia ya China.
Amesema desturi hiyo imedumu kwa miaka 28 na China ni rafiki na
mwenzi anayetegemewa zaidi na ndugu wa Afrika.
Bw. Wang pia ameeleza matarajio ya nchi yake kuhusu mkutano wa
kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mjini
Beijing mwaka huu, akisema FOCAC ni njia muhimu ya kufanya mazungumzo ya pamoja
na kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika, na pia ni
jukwaa kubwa na lenye matunda mengi zaidi kwa nchi 29 wanachama wa ushirikiano
wa Kusini na Kusini.
Amesema mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika
Johannesburg ulipata mafanikio makubwa na China inapenda kushirikiana na
marafiki wa Afrika kufanya mkutano wa mwaka huu na kuupeleka kwenye ngazi ya
juu zaidi.
Amesema
nchi nyingi za Afrika zinapongeza na kuunga mkono pendekezo la Ukanda Mmoja na
Njia Moja lililotolewa na rais Xi Jinping na China inapenda kuingiza uhai mpya
kwenye ushirikiano na Afrika kwa kupitia kujenga kwa pamoja pendekezo hilo.
Baada ya kumaliza ziara yake nchini Rwanda, Bw. Wang aliendelea
na ziara yake nchini Angola, ambapo alikutana na rais Joao Lourenco wa nchi
hiyo mjini Luanda. Bw. Wang alisema China inaiunga mkono Angola katika kutafuta
njia ya maendeleo inayolingana na hali ya nchi hiyo, kuhimiza mkakati anuwai wa
uchumi na kuongeza uwezo wa kujiendeleza.
Ameongeza kuwa China inapenda kuimarisha ushirikiano wa
kivitendo na Angola, kuinua uhusiano wa pande mbili kwenye ngazi mpya na
kupanua maeneo yatakayofanyiwa ushirikiano.
Kwa upande wake, rais Lourenco alisema ushirikiano wa pande
mbili umepata mafanikio mengi baada ya nchi hizo kuanzisha uhusiano wa kibalozi
miaka 35 iliyopita.
Ameishukuru China kutokana na uwekezaji na
msaada wake wa kifedha, ambao umefanya kazi muhimu katika kujenga amani nchini
Angola, ambako vita ilimalizika mwaka 2002 baada ya kudumu kwa miaka 27.
source CRI.
- Get link
- X
- Other Apps

Comments
Post a Comment