Waziri wa afya wa Zambia Bw. Chitalu Chilufya amesema watu 2,802 nchini humo wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu,


Waziri wa afya wa Zambia Bw. Chitalu Chilufya amesema watu 2,802 nchini humo wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu, ambapo watu 64 wamefariki kutokana na ugonjwa huo, na wengine 218 wanapatiwa matibabu.

Bw. Chilufya amesema, kuanzia leo, wizara yake itaanza kutoa chanjo ya kukinga kipindupindu kwa watu milioni 2 katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka.


Rais Edgar Lungu wa Zambia jana alitembea kituo cha matibabu ya kipindupindu kwenye uwanja wa michezo wa mashujaa wa taifa huko Lusaka, na kusema serikali itachukua hatua za kutoa maji ya kunywa na vifaa vya kuondoa takataka, ili kudhibiti kipindupindu kwa mwafaka.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.