Watu 13 wapatikana wamefungwa minyororo kwenye nyumba California

Wazazi wawili wamekamatwa huko California baada ya polisi kupata watu 13 waliokuwa wameshikiliwa mateka nyumbani kwao wakiwemo wengine waliofungiwa kwa vitanda vyao kwa minyororo na vifuli.
David Allen Turpin, 57, na Louise Anna Turpin, 49, walikamatwa kwa mashtaka ya mateso na kuhatarisha maisha ya watoto.
Watu hao 13 walio na umri wa kati ya miaka miwili na 29, walipatikana kwenye nyumna huku Peris kilomita 95 kusini mashariki mwa Los Angeles.
Wote hao wanaaminiwa kuwa ndugu.
Maafisa waligungua hilo siku ya Jumapili wakati mmoja wa watu hao alifanikiwa kuponyokana na kupiga namba ya dharura akitumia simu ambayo alipata ndani ya nyumba.
Msichana huyo ambaye polisi wanasema alionekana kuwa na umri wa miaka 10, alidai kuwa ndegu zake wengine 12 walikuwa wakishikiliwa na wazazi wao.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.