Watu 11 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya hiece kugongana na malori matatu katika kijiji cha Mubigera wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera asubuhi ya leo.



KAGERA
Watu 11 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya hiece kugongana na malori matatu katika kijiji cha Mubigera wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera asubuhi ya leo.

Gari hiyo yenye namba za usajil T.542 DKE ilikuwa ikitokea Wilaya ya Kibondo kuelekea Kahama mkoani Shinyanga, huku maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo yakiwa  chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na idadi hiyo ya vifo, na kwamba taarifa zaidi na majina itatolewa baada ya muda mfupi ili kutambua majina ya waliopoteza maisha.

Naye Mganga Mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr Grasmus Sebuyoya amethibitisha kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita, na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu












Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.