"Wasituingilie kwenye utendaji kazi" - Zambi


Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amefunguka na kusema kuwa Serikali haiwezi kupangiwa wala watumishi wake hawawezi kupangiwa kazi za kufanya na Taasisi zisizo za kiserikali wala wafadhili.
Zambi ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua utendaji wa Zahanati na vituo vya afya mkoani humo ambapo amebaini kukithiri kwa uchafu katika Zahanati hizo huku ikisemekana moja ya Asasi isiyo ya Serikali imewazuia wahudumu wa afya kufanya usafi katika Zahanati kwa madai ya kuwa kazi ya kufanya usafi si jukumu lao na kuwataka wananchi ndiyo wafanye usafi huo
.
"Naomba niseme tena kama Mkuu wa Mkoa GIZ ni wafadhili wetu tunawashukuru wanatusaidia lakini sasa wasituingilie kwenye utendaji wa kazi kwenye Zahanati zetu na vituo vya afya, mazingira yetu tunayajua sisi Zahanati iko hapa lakini mtu mwingine ana kaa kilomita mbili au tatu sasa unataka mtu huyo ndiyo aje afanye usafi halafu arudi nyumbani kwake akaendelee na majukumu mengine" alisema Zambi 
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Lindi amewataka wafadhili hao kutoingilia majukumu ya Serikali kwa kuwapangia watumishi wake namna ya kufanya kazi.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.