Wanasiasa wapewa Onyo

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni RPC, Muliro Jumanne Muliro awaonya na kuwataka wasiasa kufanya kampeni zao kistaarabu bila kuvunja sheria za nchi zinavyoelekeza na kuacha kutumia lugha zisizo na staha katika kampeni zao.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam kamanda Muliro amesema wamejipanga kuhakikisha chaguzi wa Jimbo la Kinondoni hauna nafasi yakuvunja amani na sheria za nchi kwakua taratibu na kanuni zilizowekwa na serikali zinafuatwa na hawatasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayeonekana kukiuka sheria za nchi.
Kamanda Muliro amesema wanatambua umuhimu wa zoezi hilo hivyo watagawa askari kulingana na ukubwa wa eneo na wingi wa wapiga kura.

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.