Wanao jiuza, na wanao vaa nusu utupu waanza kunywea maji kwenye karai Dar


Jeshi la Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam linaendesha oparation maalumu ya kuwakamata watu wanaofanya biashara ya kuuza mwili, pamoja na wale wanaowahifadhi kwenye nyumba zao.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda Lazaro Mambosasa ambapo amesema kufanya hivyo ni kosa kisheria na uvunjifu wa maadili hivyo ni lazima wachukuliwe hatua, pamoja na wale wanaovaa mavazi yasiyostahili kwa eneo husika.
“Kuvaa nguo fupi ni kosa la kimaadili, na sisi tunapofanya misako tunaangalia ni kosa gani limekiukwa kutokana na sheria za nchi, misako tunayoifanya tunalenga watu wanaoishi kwa kujiuza na kujipatia mapato, lakini kuvaa nguo fupi mwengine ni utamaduni wake, kwenye fukwe ukikutwa umefaaa suti tutakushangaa, lakini mtu huyo wa fukwe tukimkuta kanisani, tukimkuta msikitini tutamkamata tu”, amesema Mambosasa
Operation hiyo ya jeshi la polisi kukamata watu haitakuwa mara ya kwanza, kwani ilishawahi kufanyika siku za nyuma na kukamata baadhi ya watu wanaojihusisha na biashara hiyo

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.