Wananchi waijia juu Tanesco mkoani Katavi



MPANDA:
Baadhi ya wafanyabiashara  manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelishutumu shirika la umeme  [Tanesco] kwa kutotoa taarifa kuhusu kukatwa kwa  umeme.

Wakizungumza na mpanda redio  na wameeleza kuwa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara imekua ikisababisha kukwama kwa biashara zao hasa zinazotegemea umeme hivyo kupelekea kukosa wateja na kushindwa kujiingizia kipato.

Wafanya biashara na watumiaji umeme majumbani wanataka mamlaka kujenga kasumba ya kutoa taarifa kuhusu katizo lolote la umeme ili kuodoa usumbufu usio wa lazima.


Lakini  msemaji wa Tanesco  mkoani Katavi  ambaye amehojiwa kwa njia ya simu amedai  kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na kukatika kwa umeme  siku ya jana na usiku wa kuamkia leo.

Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa ambayo mpaka sasa inatumia majenereta kama chanzo cha nishati ya Umeme.

Source Adelina Ernest

Comments

Popular posts from this blog

SAKATA LA KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA NSIMBO MKOANI KATAVI KUKOSA DIWANI LAIBUA MJADALA MPANA

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA SERIKALI CHALI

Wanawake wa kijiji cha Kabuga kata ya Kanoge Wilayani Mpanda/Katavi wamewalaumu viongozi kwa ahadi hewa.